Tiba Asili

Tiba asili ni huduma za kiafya za kiasili zinazopatikana na kwa kila jamii kwa madhumuni ya kutambua, kukinga kutibu na kuboresha mwili kutokana na magonjwa pamoja na maradhi mbalimbali.

TIBA ASILI NI NINI?

Tiba asili ni huduma za kiafya za kiasili zinazopatikana na kwa kila jamii kwa madhumuni ya kutambua, kukinga kutibu na kuboresha mwili kutokana na magonjwa pamoja na maradhi mbalimbali. Huduma hizi zitolewazo na watu wa aina mbalimbali  kwa kutumia nyenzo, ujuzi na uzoefu wa kiasili. Tiba asilia hutofautiana toka jamii au kabila moja hadi jingine. Baadhi ya dawa au tiba toka jamii zingine zina ubora wa kipekee kiasi cha kuleta mvuto sehemu zingine.

MGANGA MAANA YAKE NINI

Kwa kawaida mganga wa tiba asili ni mtu yeyote mwenye elimu na uzoefu wa taaluma ya tiba asili ambaye anakubalika na kutambulika na jamii anamoishi, uzoefu wake wa kutoa huduma unatokana na kusomea na kurithi au kufanya kazi na mtaalamu kwenye uzoefu wa taaluma hiyo.

KAZI ZA MGANGA WA TIBA ZA ASILI

Mganga wa tiba asili aliyopata mafunzo anatarajiwa kufanya yafuatayo:-

  • Kutunza kumbukumbu za wagonjwa kwa utaratibu unaokubalika.
  • Kutambua na kuhamasisha wagonjwa wenye vidokezo vya hatari na wanaohitaji rufaa za mapema ili waende kwenye kituo cha afya husika kwa huduma ya utaaramu zaidi.
  • Kutoa huduma wakiwa wasafi.
  • Kutoa huduma katika mazingira ya usafi.
  • Kutoa elimu na nasaha kuhusu usafi, lishe bora.
  • Kutoa dawa kwa utaratibu unaokubalika
  • Kutunza vifaa vya huduma na dawa kwa utaratibu unaokubalika
  • Kushirikiana na kuwaelewa watumishi wa afya
  • Kupata mwanga juu ya misingi ya utafiti wa madawa ya asili.
  • Kushirikiana na mashirika, vikundi vyama mbalimbali hususani vya kitaaluma.
  • Kupambanua mganga wa kweli na tapeli
  • Kutoa ushauri juu ya kupunguza kasi ya kuenea kwa magonjwa hususani ya zinaa na Ukimwi
  • Kuzingatia sera, miongozo ya wizara ya afya, sheria na kanuni na taratibu za kitaaluma.

SISITIZO

  1. Waganga wajadi na wakunga wa jadi – wachane na upingaji wa ramri zinazogonganisha jamii na kukosesha amani ndani ya jamii.
  2. Watowe tiba iliyo na tija kwa jamii ili tuweze kuokoa maisha ya binadamu kwani mganga wa jadi mlishapewa karama na mwenyezi Mungu kuokoa maisha ya watu.
  3. Waganga wa jadi mnaitaji kuongeza bidii za utafiti wa madawa kwa ajili ya  kutibu magonjwa mbalimbali yaliyoshindikana kutibiwa kwenye vyombo vya kitaalam mfano Kisukari, Ukimwi, Kifafa kutoa mapepo  ambayo yamekuwa tishio kwa binadamu.
  4. Pia wananchi tunaomba nanyie ndie chanzo kikubwa cha kuleta mauaji zaidi kwa sababu unavyokwenda kwa mganga kutibiwa mna tabia ya kulazimisha waganga wawambie wachawi wenu.

MAUAJI YA KIKATIRI

Mauaji ya kikatiri – Maana yake ni kwamba watu wanachinjwa kama wanyama / kuku mfano mauaji ambayo yanayotokea mkoa wa Mara ni yakinyama, hasa wilaya ya Butiama yote imeshakuwa ya rahana kubwa. Baada ya kufanya utafiti wa kina zaidi Shimautita tuligundua kuwa watu hao wengi wao si wachawi, ni fitina za mtu na mtu anaenda kukodisha watu wakuja kwa kutumia mapanga, wengine ni fitina za mashamba, wengine ni wategaji wa samaki, mfano wavuvi wa dagaa na sangara wanaua watu sana, pamoja na machimbo kwa uchunguzi zaidi, na wengine watu wanaowaendea waganga ili kupiga ramri – za ndagu za kuua ili kupata utajiri wa haraka.

SISITIZO waganga acheni kupiga ramri kama hizo hazina maana, pia ni kudhalilisha nchi na kufanya tiba asili ikoswe thamani. Ebu angalia nchi kama China ilivyoendelea kwa madawa ya asili, tusirudishe tiba yetu ya asilia kama vile wageni walivyoingia na kuikandamiza ili ikose uthamani wake, mfano nchi ya Kijerumani na Uingereza zilikuwa hazitaki kabisa mwafrika atowe hii huduma ya tiba asili.

Ukizingatia tiba asili ilikubalika na serikali yetu toka mwaka 1974 ndipo ilianza kutambulika.

Baada ya Uhuru, tiba asilia zilikuwa chini ya Wizara ya Utamaduni mpaka mwaka 1989,  tarehe 4th  mwezi Oct mwaka 1989. Katika kikao kilichofanyika Dodoma mjini, ndipo kitengo hiki Kiliamishiwa Wizara ya afya  - na toka kiamie Wizara ya afya kina miaka 24 lakini kikawa kimeifadhiwa ofisini tu, bila mwendelezo wowote. Mpaka kufika mwaka 2001 ndipo wakaanza kutunga sera ya tiba asilia na kupitishwa kwa sera hii ya tiba asili na tiba mbadala. Bungeni na sheria ya tiba asili na kupitishwa 2002.

Sheria 23/2002 na kuzinduliwa kwa tiba ya mwafrika mwaka 2005, lakini sheria hiyo? Sheria hiyo haieleweki kwamba mpaka sasa inaranya kaiz gani?, Ombi sheria iwafikie walengwa na mabaraza yaundwe huko mikoani ili waganga waweze kutambua wajibu wa kazi zao.

USAFI NA MAZINGIRA

  1. Mganga au mkunga anahitaji kwanza mwenyewe awe msafi wa mwili mzima, aoge kabla ya kuanza kazi, nguo zake za kazi ziwe safi, ajitahidi kukata kucha zake.

Wagonjwa walazwe mahala pasafi, vyombo vya kuifadhia madawa na mahala pa kutunzia madawa pawe pasafi, wembe uwe safi.

Pia anapo fanyia kazi pawe safi, vyoo viwili vyote viwe safi mabafu yote mawili yawe safi, hadi marazi ya mganga mwenyewe yawe safi.

MADHARA YA UCHAFU

Unapokuwa unatoa huduma ukiwa mchafu basi unaweza kumuongezea mgonjwa wako magonjwa mengine, kumsababishia kuharisha, pumu, vikoozi vya kila wakati, ukimwi, pepopunda, funza, upele, ukurutu, kichocho na kunywa dawa zako bila imani anaweza kuondoka bila kupona.

KUJIKINGA NA UCHAFU ILI USIPATE MARADHI YA KUAMBUKIZWA NA MTEJA

  1. Mganga /Mkunga ni kuwa msafi kila wakati
  2. Wakati wa kutibu unatakiwa uvae gropusi mikono yote miwili.
  3. Shika wembe vizuri
  4. Mgonjwa awe na kikombe chake cha kunywea dawa anapokuwa amekaa kwa mganga.
  5. Kutozini wagonjwa wenu wakati mnaendelea kuwatibu bila Kondomu, pia hili ni kosa kubwa mno mganga akibainika na atakuwa ametenda kosa la ubakaji.

Ukibainika lazima shirika hili litakushitaki na mwananchi yeyote Yule atakaye enda kwa mganga akafanyiwa tendo hilo uende moja kwa moja kwa daktari athibitishe kisheria tuletee hiyo barua, lazima ashitakiwe na kusimamishwa kazi yake kwa kushirikiana na serikali husika.

MGANGA TAPELI

  1. Wapo watu wanaodandia na kuchafua jina la taaluma ya tiba asilia ya kitanzania.

Wapo watu wasiokuwa na taaluma ya tiba asili au wanautambuzi mdogo sana kwa taaluma hii.

Wapo wasioijua hii taaluma kazi yao ni kununua dawa kutoka kwa wataaluma, baadaye kujifanya kuwa wenyewe ndiyo wataaluma zaidi.

  • Watu hao ni wasemaji sana.
  • Hujipa sifa wenyewe
  • Hujigamba sana
  • Hujikweza
  • Husema wana weza kutibu na kuponyesha kila aina ya ugonjwa.
  • Ni wadanganyifu mno.

Hizo ni dalili za kumtambua mtapeli na wao wanajipenda sana zaidi ya mganga mwenyewe na  gharama zao ni kubwa zaidi.

MAADILI YA TIBA ASILI

Mganga wa jadi /wana taaluma wanahitaji kuzingatia maadili ya dawa, kazi zao.

  1. Unahitaji kuelewa sera na sheria za 23/2013 ya tiba asili na tiba mbadala Tanzania.
  2. Kutunza siri za wateja wako
  3. Kutozamiana / kufanya mapenzi na mteja wako.
  4. Kutokuwa muongo kiasi kikubwa.
  5. Kutoendesha shughuli zako kiutapeli
  6. Kutolewa wakati wa kutoa huduma.
  7. Kutokubaliana na mteja kulipiza visasi
  8. Kutopiga ramri za kuchonganisha ndugu na ndugu
  9. Kutonyanyasa wateja wako na kuwapiga,
  10. Timiza hivyo vipengele utaheshimika sana ndani ya jamii unamoishi.

MUNGU ALISHA TUPA UTAJILI WA KUTOSHA ALITUPENDELEA SISI WATANZANIA.

  1. Ametupa misitu mikubwa ambayo ni mali ghafi lakini hatuitumii ipasavyo.

Mizizi yote ni dawa, magome, ni dawa, majani ni dawa na chakula na mti wake ni dawa.

  1. Ametupa wanyama poli na bahari.

Vyote ni dawa ngozi, mifupa, nyama yake vyote ni dawa.

  1. Maziwa na mito vyote vilivyo samaki na maji mchanga na magugu ya ziwani, vyote ni dawa, majani ya nchi kavu ni dawa mawe ni dawa, hapo ni kwa kila mtaaluma anajua namna anavyofanyia kazi yake binafsi.

FAIDA YA DAWA ZA ASILI

  1. Inatibu na kuondoa magonjwa sugu kwa haraka
  2. Haina kemikari ya aina yeyote ile
  3. Inastawisha afya ya binadam zaidi
  4. Ina boresha mwili wa binadam zaidi na ina virutubisho vingi.

Ndugu wananchi tunaomba tuzingatie utamaduni wetu na mila na desturi usomi, dini na siasa vimepotosha mila yetu na kubakia kuthamini mila za kigeni Wananchi tugeuze akili zetu tutumie zaidi dawa zetu za asili ili tuweze kupunguza vifo vingi hapa nchini. Pia tule vyakula vya asili, mfano vyakula vyote vya nafaka na mafuta ya asili, mtaona mabadiliko ya nchi yenu kuwa makubwa kwa afya za binadam hata vifo vitapungua hapa nchini.

Mnaona magonjwa yanazidi kila kunapokucha na tiba hazipo zimebakia za wasiwasi.  Nimatumaini kuwa wananchi watabadili fikira zao ili waokowe maisha yao.

  1. Fika kwenye vituo vyetu utape huduma zilizo sahihi kwa magonjwa sugu vituo vyetu ni Musoma mjini ndipo makao makuu ya shirika yalipo.
  2. Mwanza tupo Bwiru Kijijini
  3. Kigoma - mwanga kizota, Dar es salaam – Mbagala Kuu mtaa wa mgeni nani kituo cha daladala zinapogeukia uliza steshanali ya Mwalimu Mtaki utatupata ili tukuokowe maisha yako kwa magonjwa ya aina mbalimbai yakiwemo mapepo au vipande tunatoa siku moja tu.

Pia shirika hili ni kwa kila mtu, ili mradi anapenda shughuli za maendeleo na pia ina sekta mbalimbali ndani ya katiba ya Shimautita.

SEKTA ZILIZOMO NDANI YA SHIRIKA HILI / VITENGO

  1. Waganga wa jadi, waganga wa kisasa
  2. Taasisi ya madawa ya asili
  3. Utafiti wa magonjwa ya binadamu
  4. Viongozi wa serikali na jamii
  5. Idara ya Elimu
  6. Idara ya utamaduni na mapambo
  7. Idara ya kilimo na uvuvi
  8. Idara ya mazingira
  9. Makundi rika.


 


© 2025 Shirika la Maendeleo Utafiti na Tiba Tanzania - SHIMAUTITA