Maradhi ya pumu huzuka kwa sababu ya kunywea mishipa iliyozunguka sehemu za mapafu.pia huwa ni kwa sababu ya maumbile yasiyo ya kawaida katika kifua ambayo mtoto huzaliwa nayo .Na katika hali hii maradhi huanza mapema katika maisha ya mtu.
Pumu huanza kwa kuvuta pumzi haraka haraka na kwa sauti ya kusikia.Mgonjwa wa maradhi haya anaweza kujisikia kubanwa pumzi na kutwetwa nyakati za asubuhi ,hali ambayo humfanya ang’ang’ane ili aweze kuvuta hewa . Baada ya juhudi hiyo,kufuatia kikohozi na kisha kutoa balaghamu kavu. hapo mgonjwa atajisikia nafuu kidogo.Halafu kikohozi na balagham kuendelea mpaka atakapopona.
Kuna sababu nyingi zinazosababisha mbano wa pumu,kama vile hali ya hewa kuwa baridi na kula baadhi ya vyakula kama nyama na samaki, au baada ya kula chakua kizito masaa ya jioni.Hivyo basi , kwanza mgonjwa ajue sababu ya pumu, na ajiepushe navyo vitu hivyo vinaweza kuwa maji baridi,vumbi na vinginevyo. Mgonjwa wa pumu ni lazima nyumba yake iwe na madirisha makumbwa ya kutosha.
TIBA