Kuhusu Shimautita

Shirika la Maendeleo,Utafiti na Tiba Tanzania (SHIMAUTITA) ni tasisi isiyo kuwa ya kiserikali. (NGO).Ilisajiliwa chini ya wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto. Madhumuni ya SHIMAUTITA ni   kufanya utafiti na kutoa tiba kwa magonjwa aina zote, yakiwemo yale sugu kwa kutumia dawa za mitishamba.

Wanashirika  na watumishi  wa shirika  wanatokana  na wataalamu mbalimbali wakiwemo waganga wa tiba asili ,waganga wa tiba ya kisasa na wanataaluma wengine katika masuala ya afya. Shirika linafanya kazi  kwa  ushirikiano mkubwa kati ya wataalamu wa tiba asili  na tiba za kisasa.

Makao Makuu ya shirika hili ni Musoma Mkoani Mara, Kituo kingine kipo Kwanza, Bwilu Kijijini. Kituo kingine Kigoma Mwanga Kizota, Mkoa wa Katavi wilaya ya Mpanda mjini, Dar es Salaam, Mbagala kuu – Mgeni nani, Kata ya Kijichi kwa Nyamisango au Mwalimu Mtaki.

Tunakaribisha watu mbali mbali kutoka ndani na nje ya nchi wanaopenda shughuli za maendeleo ili kuisaidia jamii. Shimautita Inawakaribisha wahisani wa aina mbali mbali, fadhili wa aina mbali mbali hata kwa mtu mmoja mmoja, pia tunakaribisha mashirika mengine wanaojishulisha na utafiti wa mitishamba, mazingira, uvuvi, kilimo, Wafugaji,  kulea watoto yatima, tunawakaribisha tuweze kushirikiana wote.

Shirika tayari limeanza kutibu magonjwa ambayo yameanishwa kwenye sehemu ya utanguli wa uchambuzi wa magonjwa. Shirika linaongozwa na uongozi wake wa shimautita wakiwa chini ya mkurugenzi mkuu Dr Machakosi C. Sinja Tanzania.

Magonjwa sugu yanayofanyiwa utafiti ni  UKIMWI (HIV/IDS),Kisukari, Polio,Kifua kikuu ,Ini, Vidonda vya tumbo, Athma, Kifafa,Kichaa,Kansa,Tauni,Kifaduro,Malaria sugu na mengineyo. Shirika limeanza kutoa tiba ya magonjwa hayo kwa uhakika zaidi .Shirika linafanya kazi zake zote kupitia  kliniki yake ijulikanayo kwa jina la Kiriba Kliniki.

Shirika linaongozwa na Mkurungezi Mtendaji, pia lina Idara kuu tatu ambazo ni :-

Idara ya Mipango,fedha na utawala.

Idara ya utafiti,madawa na uhusiano.

Idara ya tiba.

Idara hizi zinaongozwa na kurugenzi Mkuu wa Shirika.Viongozi wa shirika kwa vyeo na majina yao ni kama ifuatavyo:-

MKURUGENZI MTENDAJI                                                       -           DR. MACHOKO C. SINJA

MKURUGENZI  WA FEDHA                                                      -           GERADIA AFRIKANUS

MKURUGENZI NA UTAFITI, MADAWA NA UHUSIANO           -           THOMASI BWASABHA.

Dr .Machakosi C. Sinja  ni Mkurugenzi Mtendaji, pia ni mganga mkuu wa tiba asili na ndiye anayeongoza Idara ya Tiba asili ,akisaidiwa na Thomas Bwasabha.

Aidha shirika lina waganga wasaidizi na wakunga .Orodha kamili ni kama ilivyoorodheshwa kwenye jedwali la watumishi wa shirika.

Kwa barua, tuma
Ofisi ya Katibu Mkuu Shimautita
S. L. P 1365 Musoma

Simu: +255 (0)783 121425 | +255 (0)717 423192 | +255 (0) 753 720253

Email: shimautitatanzania@hotmail.com


 

Attachment: attachment Shimautita_Organization_Profile_2021


© 2025 Shirika la Maendeleo Utafiti na Tiba Tanzania - SHIMAUTITA