Karibu Shimautita
Shirika la Maendeleo, Utafiti na Tiba Tanzania (SHIMAUTITA) ni tasisi isiyo kuwa ya kiserikali.
(NGO). Ilisajiliwa chini ya wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto. Madhumuni ya SHIMAUTITA ni kufanya utafiti na kutoa tiba kwa magonjwa aina zote, yakiwemo yale sugu kwa kutumia dawa za mitishamba.
Wanashirika na watumishi wa shirika wanatokana na wataalamu mbalimbali wakiwemo waganga wa tiba asili ,waganga wa tiba ya kisasa na wanataaluma wengine katika masuala ya afya. Shirika linafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa kati ya wataalamu wa tiba asili na tiba za kisasa.
Magonjwa sugu yanayofanyiwa utafiti ni UKIMWI (HIV/IDS), Kisukari, Polio, Kifua kikuu ,Ini, Vidonda vya tumbo, Athma, Kifafa, Kichaa, Kansa, Tauni, Kifaduro, Malaria sugu na mengineyo. Shirika limeanza kutoa tiba ya magonjwa hayo kwa uhakika zaidi. Shirika linafanya kazi zake zote kupitia kliniki yake ijulikanayo kwa jina la Kiriba Kliniki.
Attachment:
Shimautita_Organization_Profile_2021